Jumapili 14 Septemba 2025 - 00:37
Mtafiti wa Kihindi: Umoja na mshikikano kwa Waislamu utawageuza kuwa nguvu isiyoshindwa

Hawza/ Sayyid Rashadat Ali al-Qadri katika mazungumzo yake alisisitiza kwamba umoja wa Umma wa Kiislamu una umuhimu wa juu na ni fursa yenye thamani kwa ajili ya kuimarisha mshikamano na udugu baina ya Waislamu, umoja hauwezi tu kuonesha mazingira ya kutatua matatizo ya ndani, bali pia unathibitisha nafasi halisi ya Uislamu katika uwanja wa kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Rashadat Ali al-Qadri, mtafiti wa India, katika mahojiano na mwandishi wa shirika la habari la Hawza, katika maelezo yake alisisitiza kwamba umoja kwa Umma wa Kiislamu ni fursa yenye thamani ya kuimarisha mshikamano na udugu baina ya Waislamu na unaweza kwa pamoja kutoa mazingira ya kuondoa matatizo ya ndani na pia kuthibitisha nafasi halisi ya Uislamu katika uwanja wa kimataifa.

Yafuatayo ni maelezo ya mahojiano haya:

Kwa kuzingatia hali yenye changamoto kubwa ya leo, umuhimu wa umoja unaweza kutathiminiwa vipi?

Sayyid Rashadat Ali al-Qadri: Leo hii jamii ya Kiislamu inakabiliana na matatizo na migogoro mingi; kuanzia mvutano wa kisiasa na mashindano ya madaraka hadi mashinikizo ya kiuchumi na hata mipasuko ya kijamii, katika hali kama hii, umoja unatukumbusha ukweli huu kwamba ni kwa mshikamano na mshikikano pekee ndipo tunaweza kushinda matatizo haya, bila umoja umma wa Kiislamu utabaki dhaifu mbele ya mashambulizi; lakini kwa mshikikano, uwezo wa kukabiliana na changamoto yoyote utapatikana.

Una tathmini vipi hali ya mgawanyiko na mtengano ndani ya Umma wa Kiislamu?

Sayyid Rashadat Ali al-Qadri: Mgawanyiko kwa hakika ni hasara kubwa zaidi kwa Umma wa Kiislamu. Kila mara tofauti na utengano vinapojitokeza baina ya Waislamu, nguvu na uwezo wao huanza kudhoofika na maadui hunufaika ipasavyo na fursa hii, wakati ambapo ujumbe mkuu wa Uislamu umejengeka juu ya mapenzi, mshikamano na udugu. Ikiwa Waislamu wataweza kuutekeleza msingi huu muhimu katika maisha yao binafsi na ya kijamii, basi Umma wa Kiislamu utageuka kuwa nguvu imara na isiyoshindwa.

Kwa mtazamo wako, ni hatua zipi kivitendo zinaweza kusaidia kuimarisha na kuthibitisha umoja?

Sayyid Rashadat Ali al-Qadri: Hatua ya kwanza ni kuimarisha utamaduni wa uvumilivu, kustahamiliana na kuelewana. Tofauti za maoni na mitazamo ni jambo la kimaumbile, lakini tofauti hizi hazipaswi kupelekea ugomvi, njia sahihi ni mazungumzo, maelewano na kutafuta suluhisho ya pamoja, hatua ya pili ni kuzingatia kizazi cha vijana. Ni lazima kupitia malezi sahihi, kueneza utamaduni wa Kiislamu na kusisitiza juu ya thamani za kibinadamu, kizazi kijacho kifahamishwe kwa malengo ya umoja, ikiwa wao watakuzwa katika njia ya udugu na mshikamano, basi mustakabali wa Umma wa Kiislamu utakuwa wenye nuru.

Mwisho, umoja una ujumbe na maana gani kwa Umma wa Kiislamu?

Sayyid Rashadat Ali al-Qadri: Ujumbe wa umoja ni wa wazi kabisa: Sote ni sehemu ya Umma mmoja, tuna Qibla kimoja na ni lazima tusimame katika safu moja thabiti na yenye mshikamano, umoja baina ya Waislamu hauwezi tu kutoa mazingira ya kutatua matatizo na changamoto za ndani, bali pia unaongeza nguvu na uwezo wao wa kutekeleza nafasi yao halisi katika uwanja wa kimataifa, wakati Waislamu wanaposhikamana mikono na kutembea kwa mshikamano, wanaweza kuthibitisha nafasi ya kweli ya Uislamu duniani na kuonesha ukubwa wa kweli wa dini hii.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha